Ni kweli
kuwa karibu vitabu vyote vya dini vinasisitiza kuwa na mwenza wa maisha kama
njia sahihi ya kuishi maisha yako ya kimapenzi na pia kutimiza majukumu mengine
ya kuendelezana kati ya jinsia hizo mbili. Katika makala hii mambo ya msingi ya
kuepuka ili upate mke atakayekidhi maelekezo ya vitabu vya dini, yaani mke
bora. Kabla ya kuenda mbali tujikumbushe vitabu vinasema nini kuhusu mke bora:
"Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri."--Qur'an 30:21 http://www.theholyquran.org/
Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.- Mithali 18:22 https://www.wordproject.org
Sintokuchosha na mistari mingi toka vitabu vya dini, hiyo
miwili hapo juu inatosha kueleza ubora na umuhimu wa kupata mwenza sahihi wa
ndoa. Hata hivyo swali gumu linalowakwamisha wengi ni kuwa je unamjua mwanamke
atakayeweza kuwa mke mwema ?
Usitegemee kumrekebisha wakati mmeshaoana:
Ndoa sio uwanja
au shule ya mafunzo kwa mke wako kuishi unavyotaka hivyo usitegemee kuoa mke
mwenye tabia fulani usizozipenda kwa kujipa moyo akiwa katika ndoa
atajirekebisha. Je asipojirekebisha ? Hapo ndo mwanzo wa migogoro isiyoisha.Unamkubali
mke maana yake umemchunguza na kusema “namkubali” , na kama kuna madhaifu basi
maana yake umekubali kuishi nayo kwani hata wewe pia una madhaifu yako.
Anaonyesha vitendo sio tuu maneno:
Ni zaidi ya kuwa mcha
Mungu kwa maana ya muonekano wa kuenda msikitini au kanisani, bali anaonyesha
vitendo kuwa ni mwenye huruma, mpole kiasi, na mwenye kuthamini wengine.
Sio mfuata
upepo:
Mke bora ana uhuru wa fikra sio
tuu dhidi ya wewe kukubaliana na kila jambo unalotaka , ila pia anakuwa na
uwezo wa kuchambua anayoyasikia toka nje ya ndoa yenu na kubaki na mtazamo
chanya wa mahusiano yenu. Hata kwa wewe mwenyewe hatokuwa mfuata upepo wa kila
utakacho kwani kumbuka kuwa yeyé ni msaidizi wako, hivyo kuwa tayari pale
atakapokurekebisha na kukukosoa .
Mdadisi na
mwenye kujifunza
Nyote mnapoanza mahusiano mnakuwa na ndoto ya maisha ya
furaha na mafanikio. Hata hivyo kadri siku zinavyoenda na mabadiliko ya kijamii,
kiuchumi, na nyie wenyewe pia mnabadilika kitafakari na kimahitaji. Mke bora atapenda kuwa mdadisi
na kujifunza kukabiliana na mabadiliko haya ili kuendelea kutunza ndoa yake.
Mmejadili naye
mambo ya msingi kuhusu maisha yenu ya baadae na unafahamu msimamo wake
Katika
makala yetu ya siku za nyuma
tulijadili kuwa kuna mambo 6 yanayoweza
kuhatarisha mahusiano yenu kama hamtojadili na kufikia muafaka. Mambo hayo ni
fedha, imani, mahala pa kuishi, watoto, falsafa ya maisha na hisia za mapenzi. Soma zaidi BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment