Saturday, March 28, 2015

UMUHIMU WA KUSOMEA ELIMU YA SOFTWARE

Katika ulimwengu ambao karibu kila kitu kinaendeshwa kwa Software, yaani program mbalimbali za kompyuta, bila shaka wenye kuzalisha na kumiliki hizo software na vyombo vya elektronik ndio wenye nguvu ya kiuchumi, kisiasa na kitamaduni.
Hata hivyo tujiulize ni kwa kiwango gani ndani ya bongo yetu tumeweka mkazo katika kuwafanya watu wengi zaidi kuipenda na kujikita kwenye kuzalisha software.

Tupo katika ulimwengu ambao nyenzo nyingi za kukuwezesha kujikita katika software ni BUREEEE. Iwe unataka kutengeneza mobile apps, au desktop apps, au tuu unataka kubobea kwa website.

Badala ya kutumia kompyuta kama chombo cha "kupoteza muda" , waweza jifunza mambo mengi ya kukufanya uwe mzalishaji katika ulimwengu wa digitali.
Badala ya kuweka msisitizo katika kuwa watumiaji na wanunuzi katika ulimwengu wa digital, tuanze kampeni ya kuhimiza kuanzia watoto kupenda kuwa watundu na wazalishaji wa bidhaa za kidigital. 
Nchi za wenzetu , wataalamu wa fani hii huanzia wakiwa wadogo sana.

0 comments:

Post a Comment