![]() |
Dexter Morgan katika tamthilia iitwayo DEXTER anaonyesha tabia zinazotambulisha Sociopaths. Itazame hiyo tamthilia kwa kujiongezea ujuzi kuhusu watu hawa hatari waitwao sociopaths. |
Hii ni kwa mujibu wa mtaalamu aitwaye Paul Rosenberg na
references nyingine. Atakayetaka makala nzima aniambie email yake ntamtumia.
Kwanza sociopath ni nani ? A sociopath: is an otherwise normal human who has a profound lack of empathy for the feelings of others. Yaani sociopath kwa asili yeye haoni huruma kwa mtu yoyote yule. Hata hivyo sio lazima ajionyeshe wazi wazi kuwa hana huruma, hujificha ili kutimiza hitaji lao la kumpata mtu wa kumtenda.
Kwanza sociopath ni nani ? A sociopath: is an otherwise normal human who has a profound lack of empathy for the feelings of others. Yaani sociopath kwa asili yeye haoni huruma kwa mtu yoyote yule. Hata hivyo sio lazima ajionyeshe wazi wazi kuwa hana huruma, hujificha ili kutimiza hitaji lao la kumpata mtu wa kumtenda.
Kwakuwa wao hawana hisia zozote za huruma wala mapenzi,
inawalazimu hao sociopath kuiga watu wa kawaida wanavyoishi. Na kwakuwa
hatutilii maanani jinsi watu wanavyoonekana , ni ngumu kutambua nani haswa ni
sociopath, nani siye.
Ni shida
kumjua sociopath kwakuwa
1. Wengi
wetu tunaamini kila mtu ni mzuri, wakati ukweli kuna watu 100% ni wabaya tuu,
ni muda tuu unawasubirisha kufanya ubaya wao.
2. Sio
wengi sana inakadiriwa 2% ya watu wote ni sociopath mahesabu ambayo pia
yanasemwa kuwa kati ya watu 50 mmoja ni sociopath
3. Lingine
kwakuwa wao hawana hisia yoyote wao hawajisikii vibaya kudanganya, jambo
linawapelekea kutokutambulika uongo wao hata kwenye LIE DETECTERS, zile mashine
za kutambua kama mtu anasema uongo au la.
Baada ya
kueleza hapo juu kwanini ni ngumu kwa watu wengi kumtambua sociopath tuone
jinsi ya kumtambua.
1. Kama
unasoma hii kitu tayari unafaida ya kumtambua sociopath kwakuwa wao hutumia
kutokujua kwetu kuwa wao wapo. Ile imani kuwa kila mtu mzuri hutuharibu na
kutuweka hatarini kudhurika na sociopath. Hivyo kila wakati tambua kusoma jinsi
mtu anavyobehave.
2. Pamoja
na kwamba sociopath huiga kuonekana wapo wa kawaida, huwa wanashindwa kwa
asilimia 100 kuonyesha huruma na upendo. Ingawa wengine huwa na wenza wa ndoa,
na hata watoto, ila chunguza namna wanavyoonyesha hisia zao haswa utagundua
utofauti mkubwa. Vitu vya kuangalia ni namna wanavyojali wapenzi wao, watoto,
mambo ya misiba na mijumuiko ya kijamii,
pamoja na kuweza kufeki, ila ukia ngalia kwa makini utajua kuna
walakini.
3. Kwakuwa
sociopath kiasili hujisikia raha kudhuru wengine , chunguza watu ulionao
karibu je hujisikia raha kusingizia
wengine, au hufanya matendo yasiyo ya
kihuruma na hawaonyeshi kujutia, n.k .
4. Wazungu wanasema "when the deal is so good, think
twice". Kuwa makini na watu wanaojifanya wema sana.
5.Kwakuwa wanahitajika kujificha, hujitengenezea mazingira
ya kutokutambulika na kuiaminisha jamii kuwa ni watu safi, kiasi kwamba hata
ukija sikia wamefanya hivyo utashangaa. Wengi wa wanasiasa na viongozi wa
asasi mbalimbali inasemekana ni sociopath.
Chunguza
maamuzi ya wanasiasa wengi yasivyo na huruma. Mfano wa viongozi maarufu ni Mao
Tse-tung ambaye ni baba wa taifa la
CHINA anayedaiwa kubaka na kuua watu wengi kwa njaa. Mwingine ni
kiongozi wa zamani wa shirika la utangazaji la BBC anaitwa Jimmy Savile ,yeye
alikuwa na genge la udharirishaji wa watoto. Aliendesha genge lake kwa miaka 40
bila watu kujua, mpaka alipofariki.
Baadhi ya
maswali ambayo watu wengi huuliza:
Je unajitambua kama wewe ni Sociopath ?
Waweza
jipima kama wewe ni sociopath au la. Je, unapata ugumu kuwaonea wengine huruma
? Je unapenda kuona wengine wanateseka au haujisikii lolote mtu mwingine
anapoteseka ? Je, kwa makusudi umewahi kutaka kumfanyia "kitu mbaya" mtu
?
Je, sociopath kuna kitu kinatokea unakuwa
triggered?
Sio lazima kitu kitokee wawe triggered, kumbuka hawa
sociopath hawana hisia zozote
Je sociopath ni
wazungu tuu kwa kuwa wazungu labda wanakuwa lonely so hawana cha kufanya kiasi
kwamba wananyemelewa na hizo hisia?
Sociopath hajisikii lonely. Hajui hizo hisia za kuwa lonely
, hajisikii kutaka kupendwa, hajisikii chochote. Huyo ndio real sociopath. Hata hivyo SIO kila mtu mwenye kufanya jambo la
ukatili ni sociopath. Kuna wanaofanya jambo baya wakajutia, pengine kwa hasira
, au visasi. Ila sociopath yeye , kufanya ubaya ni "hitaji"
lake muhimu.
Serial Killers wote ni sociopath. Serial killers ni wale
wanaojitengenezea orodha ya. watu wanaowaua. Ni hatari sana hawa watu, kwani
sio lazima watumwe kuua. Ni kwamba wanajitengenezea sababu zao kichwani mwao
zinazowatosha basi.
Hata hivyo SIO kwamba sociopaths wote ni serial killers.
Hata hivyo SIO kwamba sociopaths wote ni serial killers.
Nchini kenya kuna sociopath mmoja alikuwa akiwaua watu na kunywa damu yao...lakini alishikwa sahizi anatumikia kifungo. Alikuwa maafuru na anajulikana kwa jina Onyancha. Hawa watu ni wabaya aisee
ReplyDelete