Jitahidi uwe mdadisi wa habari unazoziona mtandaoni zikakuogopesha au zikakutaka ufanye maamuzi fulani makubwa kuhusu maisha yako. Kuna aina mbili za habari nataka kuzizungumzia leo:
1. Habari za Uzushi : Zinaitwa kwa kizungu HOAX. Mfano wa habari hizo ni kama ile iliyosema John Cena kafariki ktk ajali au mfano wa nyingine zinakutaka kushare taarifa na watu wengine ili wasidhurike.
2. Kuna habari zingine SIO uzushi,ila huonekana kama maajabu hivyo kufanya watu waogope kuwa mwisho wa dunia umekaribia. Ila ukweli ni kuwa habari hizo zinaelezea hali ambazo ni nadra kutokea ila zinawezekana kutokea na kuna maelezo ya kisayansi kwanini hutokea. Ila kwa ufahamu wa wengi haiwezekani hivyo kuchukulia ni jambo la kutia hofu. Mfano mzuri ni habari za mionekano ya picha za Yesu kwenye mawingu, au maandishi ya kidini hata ya kiislamu. Nyingine ni mvua zinazodosha vitu kama samaki, nyanya, chura na hata imewahi kutokea mvua ya matope!
Hivyo kabla haujasambaza habari au kuingiwa na woga , jaribu kufanya utafiti , mambo mengi unayoogopa kwa sababu ya kutoyafahamu pengine hofu itaondoka ukipata ufahamu sahihi.
0 comments:
Post a Comment