Sunday, April 19, 2015

PICHA FEKI ZA VURUGU HUKO AFRIKA KUSINI


Fake South African xenophobic photo


Kuna picha ambayo imesambaa sana ikuhusisha matukio ya wiki hii ya vurugu na kuuawa kwa wageni huko Afrika Kusini. Hata hivyo picha hiyo imekuwepo mtandaoni kwa muda mrefu hata kabla ya matukio ya hivi karibuni. 
Uki"google" picha za mwaka 2012, hiyo picha inaonekana ktk baadhi ya taarifa mbalimbali ikuhusisha ktk habari moja mwizi kuchomwa moto, nyingine ikisema mchawi, na nyingine ikiuliza ipi bora kuchomwa moto au kuzamishwa kwenye maji. 
Tunapinga kwa nguvu zote vurugu , mauaji na ubaguzi wa wageni SA. 
Ila tukumbuke sio kila habari, picha na videos tunaziona mtandaoni zina ukweli. Hapa chini ni hiyo picha, bila shaka umeiona ikihusisha matukio ya hivi karibuni huko Sauzi.

0 comments:

Post a Comment